sw_tw/bible/other/yoke.md

566 B

Nira

Ufafanuzi

Nira ni kipande cha mbao au chuma kinachowekwa kwa wanyama wawili au zaidi ili kuwaunganisha kwa ajili ya lengo la kuvuta plau au gari.

  • Pia nira imetumika kuelezea kitu kilichowaunganisha watu kwa ajili ya lengo la kufanya kazi pamoja kwa mfano kumtumikia Yesu.
  • Paulo anatumia neno "mjoli" kumaanisha mtu anayemtumikia Yesu kama alivyo.
  • Neno "nira" pia linaweza kutumika kama mzigo mzito ambao mtu anaubeba kwa mfano anayetumikishwa utumwani au kwenye mateso.
  • Namna nyingine ya kutafsiri neno hili waweza kutumia neno "mzigo mzito".