sw_tw/bible/other/wine.md

13 lines
780 B
Markdown

# Divai, kiriba, divai mpya
## Ufafanuzi
Katika nyakati za Biblia "divai" ni kinywaji kilichotengenezwa na maji ya matunda yanayoitwa zabibu. Divai ilihifadhiwa kwenye viriba ambayo ni vyombo vilivyotengenezwa kwa ngozi ya wanyama.
* Divai mpya ni maji ya zabibu ambayo hayajatolewa bado kwenye zabibu.
* Kutengeneza divai zabibu hupondwa kwenye shinikizo na maji ya zabibu hutoka ndani yake. Maji haya huchachushwa na kuleo hutoka ndani yake.
* Katika nyakati za Biblia divai kilikuwa kinywaji cha kawaida kikiambatana na mlo. Haikuwa na kilevi sana kama divai za wakati huu.
* Kabla divai haijawekwa kwa ajili ya kutumika ilichanganywa na maji.
* Viriba vilivyochakaa vilikuwa vimepasuka na kuruhusu divai kuvuja. Lakini viriba vupya havikuvuja na vilihifadhi divai vizuri.