sw_tw/bible/other/wine.md

780 B

Divai, kiriba, divai mpya

Ufafanuzi

Katika nyakati za Biblia "divai" ni kinywaji kilichotengenezwa na maji ya matunda yanayoitwa zabibu. Divai ilihifadhiwa kwenye viriba ambayo ni vyombo vilivyotengenezwa kwa ngozi ya wanyama.

  • Divai mpya ni maji ya zabibu ambayo hayajatolewa bado kwenye zabibu.
  • Kutengeneza divai zabibu hupondwa kwenye shinikizo na maji ya zabibu hutoka ndani yake. Maji haya huchachushwa na kuleo hutoka ndani yake.
  • Katika nyakati za Biblia divai kilikuwa kinywaji cha kawaida kikiambatana na mlo. Haikuwa na kilevi sana kama divai za wakati huu.
  • Kabla divai haijawekwa kwa ajili ya kutumika ilichanganywa na maji.
  • Viriba vilivyochakaa vilikuwa vimepasuka na kuruhusu divai kuvuja. Lakini viriba vupya havikuvuja na vilihifadhi divai vizuri.