sw_tw/bible/other/unlawful.md

12 lines
826 B
Markdown

# kinyume cha sheria
## Ufafanuzi
Maneno "kinyume cha sheria" na "sio kisheria" yanatumika kueleza matendo yanayo vunja sheria.
* Katika Agano Jipya, neno "kinyume cha sheria" sio tu la tumika kueleza kuvunja amri ya Mungu, bali pia kuvunja sheria za Kiyahudi.
* Baada ya miaka, Wayahudi waliongeza kwenye sheria Mungu alizowapa. Viongozi wa Kiyahudi waliita kitu "kinyume cha sheria" kama hakikuendana na sheria zao wao.
* Yesu na wanafunzi wake walipo kuwa wana nyofoa nafaka siku ya Sabato, Mafarisayo waliwashtaki kufanya "kinyume cha sheria" kwasababu ilikuwa ina vunja sheria za Wayahudi za kutofanya kazi hiyo siku.
* Wakati Petro alipo sema kula chakula najisi ni "kinyume cha sheria" kwake, alimaanisha kama angekula vyakula angekuwa na vunja sheria Munug alizo wapa Waisraeli kuhusu kuto kula baadhi ya vyakula.