728 B
728 B
Kimbilio, malazi
Ufafanuzi
"Kimbilio" ni sehemu au hali ya usalama na ulinzi. "Malazi" ni sehemu yenye muundo wa kimwili ambayo inakulinda kutokana na hali ya hewa au hatari.
- Katika Biblia Mungu anaelezwa kama kimbilio ambapo watu wake huwa salama na kupata ulinzi kwake.
- "Mji wa makimbilio" katika agano la kale ni miji ambayo mtu akiua kwa bahati mbaya hukimbilia huko kwa ajili ya usalama toka kwa watu wanaotaka kumvamia na kulipa kisasi.
- Malazi ni sehemu inayojengwa kama jengo ambalo laweza kutoa ulinzi kwa watu au wanyama.
- Mara nyinginge malazi humaanisha usalama. Lutu aliposema wageni wake wapo chini ya malazi ya paa lake alikuwa na maana kuwa walikuwa salama kwa sababu walikuwa kwenye nyumba yake.