sw_tw/bible/other/proud.md

463 B

Kiburi

Ufafanuzi

Kiburi ni hali ya mtu kujifikiria mwenyewe na kudhani kuwa yeye ni bora kuliko wengine.

  • Mtu mwenye kiburi huwa hakubali makosa yake. Sio mnyenyekevu.
  • Kiburi kinaweza kusababisha usimtii Mungu katika njia nyingine.
  • Pia kiburi kinaweza kuelezwa katika mtazamo chanya kwa mfano "kujivunia" kwa kitu ambacho mtu fulani amefanikiwa au "kujivunia" watoto wako.
  • Mtu anaweza kujivunia kwa alichokifanya bila kuwa na kiburi juu ya hilo.