sw_tw/bible/other/praise.md

13 lines
443 B
Markdown

# Kusifu
## Ufafanuzi
Kumsifu mtu ni kuonesha pongezi au heshima kwa mtu yule.
* Watu wanamsifu Mungu kwa namna alivyo mkuu na kwa sababu ya mambo ya ajabu anayoyafanya kama muumbaji na mwokozi wa dunia.
* Kumsifu Mungu kunajumuisha kumshukuru kwa aliyoyafanya.
* Muziki na kuimba hutumiwa kama njia ya kumsifu Mungu.
* Kumsifu Mungu ni sehemu ya kumwabudu.
* Neno "kusifu" yaweza kutafsiriwa kama "kusema mazuri" au "kusifia kwa maneno."