sw_tw/bible/other/praise.md

443 B

Kusifu

Ufafanuzi

Kumsifu mtu ni kuonesha pongezi au heshima kwa mtu yule.

  • Watu wanamsifu Mungu kwa namna alivyo mkuu na kwa sababu ya mambo ya ajabu anayoyafanya kama muumbaji na mwokozi wa dunia.
  • Kumsifu Mungu kunajumuisha kumshukuru kwa aliyoyafanya.
  • Muziki na kuimba hutumiwa kama njia ya kumsifu Mungu.
  • Kumsifu Mungu ni sehemu ya kumwabudu.
  • Neno "kusifu" yaweza kutafsiriwa kama "kusema mazuri" au "kusifia kwa maneno."