18 lines
995 B
Markdown
18 lines
995 B
Markdown
# mfalme
|
|
|
|
## Ufafanuzi
|
|
|
|
Neno "mfalme" linamaanisha mwanamme ambaye ni mtawala mkuu wa mji, jimbo, au nchi.
|
|
|
|
Mfalme kawaida huchaguliwa kutawala kwa sababu ya uhsiano wake kifamilia na wafalme wa nyuma.
|
|
Mfalme anapokufa, kawaida mwana wake mkubwa ndiye anayekuwa mfalme mpya.
|
|
Katika nyakati za zamani, mfalme alikuwa na mamlaka yote juu ya watu katika ufalme wake.
|
|
Neno "mfalme" halitumiki sana kwa mtu asiye mfalme wa kweli, kama "mfalme Herode" katika Agano Jipya.
|
|
Katika Biblia, Mungu anajulikana kama mfalme anaye tawala juu ya watu wake.
|
|
"Ufalme wa Mungu" unamaanisha utawala wa Mungu juu ya watu wake.
|
|
Yesu aliitwa "Mfalme wa Wayahudi," "mfalme wa Israeli," na "mfalme wa wafalme."
|
|
Yesu atakaporudi, atatawala kama mfalme wa dunia.
|
|
Neno hili linaweza kutafsiriwa kama, "mkuu" au "kiongozi kamili" au "mtawala mwenye nguvu."
|
|
Usemi "mfalme wa wafalme" unaweza kutasiriwa kama "mfalme anayetawala juu ya wafalme wengine wote" au "kiongozi mkuu aliye na mamlaka juu ya viongozi wengine wote."
|
|
|