25 lines
1.7 KiB
Markdown
25 lines
1.7 KiB
Markdown
# mkono, mkono wa kuume,
|
|
|
|
## Ufafanuzi
|
|
|
|
Neno 'mkono' limetumika katika Biblia kama lugha ya picha kwa njia mbalimbali
|
|
Kuweka kitu katika mikono ya mtu fulani inamaana ya kukabidhi kitu hicho.
|
|
Neno 'mkono' limetumika kurejelea uweza au nguvu ya Mungu na matendo yake. kwa mfano, Mungu anaposema "je si mkono wangu uliyoyafanya haya?"
|
|
Neno "kabidhi" hurejelea maana ya kuweka kitu katika mkono au utawala wa mtu fulani.
|
|
Kuweka mikono juu ya mtu fulani mara nyingi huambatana na utoaji wa baraka kwa mtu huyo.
|
|
Pia kitendo cha 'kuweka mikono" juu ya mtu kinamaanisha kumweka mtu huyo wakfu kwa ajili ya kazi ya Mungu au kwa ajili ya kumwombea mtu huyo uponyaji.
|
|
Baadhi ya lugha za picha za neno mkono ni:
|
|
Kunyosha mkono juu ya mtu maana yake ni kumdhuru.
|
|
''kumwokoa kutoka katika mkono wa..." ni kumzuia mtu ili asimdhuru mtu mwingine.
|
|
matumizi mengine ya mkono ni kama:
|
|
"kunyosha mkono" ina maana ya 'kudhuru' au kuumiza"
|
|
"kumwokoa mtu mikononi mwa" ina maana ya kumzuia mtu ili asimdhuru mtu mwingine.
|
|
"kuwa karibu na mkono " kuwa 'karibu'
|
|
"kuwa mkono wa kuume" humaanisha kuwa 'nafasi'' au ''sehemu ya'' au "upande wa kulia"
|
|
Maelezo yanayosema "kwa mkono wa'' au ''kupitia mkono'' ina maana kuwa kitendo kimefanya na mtu huyo. kwa mfano, "kwa mkono wa Bwana'' ina maana kuwa Bwana ndiye amefanya tendo hilo.
|
|
Wakati Paulo anasema " imeandikwa kwa mkono wangu" ina maana kuwa sehemu hii ya barua iliandikwa kwa mkono wake kabisa, badala tu kusema na mtu mwingine akayaandika.
|
|
|
|
Mapendekezo ya tafsiri.
|
|
Maelezo haya na tamathali hizi za semi zaweza kutafsiriwa kwa kutumia lugha zingine za picha ambazo zina maana sawa. Au maana inaweza kutafsiriwa kwa kutumia lugha ya moja kwa moja.
|
|
|