sw_tw/bible/other/festival.md

23 lines
788 B
Markdown

# sikukuu
## Ufafanuzi
Kwa ujumla, sikukuu ni sherehe iliyofanyika na jamii ya watu.
Neno kwa ajili ya "sikukuu" katika Agano la Kale lina maana ya "muda ulioteuliwa".
Sikukuu zinazosherehekewa na Waisraeli zilikuwa nyakati maalumu zilizoteuliwa au nyakati ambazo Mungu aliwaamuru wao kuzifuata.
Katika baadhi ya tafasiri za Kiingereza, neno "sikukuu" linatumika badala ya karamu kwa sababu sherehe zilijumuisha mlo mkubwa wa pamoja.
Kulikuwa na karamu kadhaa ambazo Waisraeli walisherehekea kila mwaka:
Pasaka
Sikukuu ya Mkate Usiotiwa Chachu
Mavuno ya Kwanza
Sikukuu ya Wiki (Pentakuki)
Sikukuu ya Tarumbeta
Sikukuu ya Kulipia Kosa
Sikukuu ya Vibanda
Kusudi la sikukuu hizi ilikuwa kumshukuru Mungu na kukumbuka mambo ya ajabu aliyofanya kuwaokoa, kuwalinda na kuwapa watu wake.