sw_tw/bible/other/clan.md

12 lines
429 B
Markdown

# Ukoo
## Ufafanuzi
Ukoo ni kundi la wana familia wanaotokana na mababu.
* Katika agano la kale Waisraeli walihesabiwa kutokana na koo zao au makundi ya familia.
* Koo zilipewa majina kutokana na babu aliyejulikana sana.
* Mtu mmoja mmoja mara nyingine huitwa kwa jina la ukoo wake. Kwa mfano baba mkwe wa Musa mara nyingine aliitwa kwa jina la ukoo wake Reueli.
* Ukoo waweza kutafsiriwa kama "kundi la familia" au "ndugu."