sw_tw/bible/other/barley.md

12 lines
466 B
Markdown

# shayiri
## Ufafanuzi
Neno "shayiri" limamaanisha aina ya nafaka iliyokuwa ikitumika kutengeneza mkate.
* Mche wa shayiri una bua refu lenye suke juu yake ambamo ndani yake punje au nafaka inakua.
* Shayiri hustawi wakati wa joto hivyo kwa kawaida inavunwa wakati wa kiangazi.
* Wakati shayiri inapopurwa, mbegu ya kuliwa inatenganishwa na makapi.
* Nafaka ya shayiri inasagwa na kuwa unga, ambao hatimaye unachanganywa na maji na mafuta ili kutengeneza mkate.