sw_tw/bible/other/assembly.md

12 lines
656 B
Markdown

# Mkutano, kukusanyika
## Ufafanuzi
Mkutano ni kundi la watu wanaokusanyika pamoja kujadili matatizo, kupeana ushauri na kufanya maamuzi.
* Mkutano ni kundi la watu wanaokusanyika pamoja kwa mda mfupi kwa ajili ya jambo maalumu au tukio maalumu.
* Katika agano la kale kulikuwa na mkutano maalumu ulioitwa mkutano takatifu ambapo wana wa Israeli walikusanyika kumuabudu Yahweh.
* Mara nyingine mkutano ina maanisha Waisraeli kwa ujumla kama kundi.
* Katika agano jipya viongozi wa Kiyahudi 70 katika miji mikuu kama Yerusalemu walikusanyika ili kutatua masuala ya kisheria na kutatua migogoro kati ya watu. Mkutano huo ulikuwa unajulikana kama Baraza.