sw_tw/bible/other/assembly.md

656 B

Mkutano, kukusanyika

Ufafanuzi

Mkutano ni kundi la watu wanaokusanyika pamoja kujadili matatizo, kupeana ushauri na kufanya maamuzi.

  • Mkutano ni kundi la watu wanaokusanyika pamoja kwa mda mfupi kwa ajili ya jambo maalumu au tukio maalumu.
  • Katika agano la kale kulikuwa na mkutano maalumu ulioitwa mkutano takatifu ambapo wana wa Israeli walikusanyika kumuabudu Yahweh.
  • Mara nyingine mkutano ina maanisha Waisraeli kwa ujumla kama kundi.
  • Katika agano jipya viongozi wa Kiyahudi 70 katika miji mikuu kama Yerusalemu walikusanyika ili kutatua masuala ya kisheria na kutatua migogoro kati ya watu. Mkutano huo ulikuwa unajulikana kama Baraza.