sw_tw/bible/names/zebedee.md

10 lines
385 B
Markdown

# Zebedayo
## Ufafanuzi
Zebedayo alikuwa mvuvi kutoka Galilaya anayejulikana kwa sababu ya wanawe, Yakobo na Yohana, waliokuwa wanafunzi wa Yesu. Hawa wamekuwa wakitajwa katika Agano Jipya kama "wana wa Zebedayo."
* Wana wa Zebedayo walikuwa wavuvi pia na walifanya naye kazi ya kuvua samaki.
* Yakobo na Yohana waliacha kazi yao ya kuvua na Zebedayo baba yao na wakamfuata Yesu.