sw_tw/bible/names/paul.md

15 lines
913 B
Markdown

# Paulo, Sauli
## Ufafanuzi
Paulo alikuwa kiongozo wa kanisa la kwanza aliyetumwa na Mungu kupeleka habari njema kwa makundi mengi ya watu.
* Paulo alikuwa Myahudi aliyezaliwa Rumi kwenye mji wa Tarso hivyo alikuwa raia wa Rumi.
* Paulo kwa jina la Kiyahudi aliitwa Sauli.
* Sauli alikuwa kiongozi wa dini ya Kiyahudi na aliwafunga Wayahudi waliokuwa Wakristo kwa sababu alifikiri kuwa hawakumuheshimu Mungu kwa kumwamini Yesu.
* Yesu alijidhihirisha mwenyewe kwa Sauli kwa kutumia mwanga unaopofua na kumwambia aache kuwatesa Wakristo.
* Sauli alimwamini Yesu na akaanza kuwahubiria Wayahudi wenzake kuhusu Yesu.
* Baadaye Mungu akamtuma Sauli kwenda kuwahubiria wasio Wayahudi kuhusu Yesu na kuanzisha makanisa katika miji na vijiji mbalimbali. Wakati huu sasa akaanza kuitwa Paulo.
* Paulo pia aliandika barua ili kuwatia moyo Wakristo katika makanisa kwenye miji hiyo. Barua hizi zipo katika agano jipya.