sw_tw/bible/names/paul.md

913 B

Paulo, Sauli

Ufafanuzi

Paulo alikuwa kiongozo wa kanisa la kwanza aliyetumwa na Mungu kupeleka habari njema kwa makundi mengi ya watu.

  • Paulo alikuwa Myahudi aliyezaliwa Rumi kwenye mji wa Tarso hivyo alikuwa raia wa Rumi.
  • Paulo kwa jina la Kiyahudi aliitwa Sauli.
  • Sauli alikuwa kiongozi wa dini ya Kiyahudi na aliwafunga Wayahudi waliokuwa Wakristo kwa sababu alifikiri kuwa hawakumuheshimu Mungu kwa kumwamini Yesu.
  • Yesu alijidhihirisha mwenyewe kwa Sauli kwa kutumia mwanga unaopofua na kumwambia aache kuwatesa Wakristo.
  • Sauli alimwamini Yesu na akaanza kuwahubiria Wayahudi wenzake kuhusu Yesu.
  • Baadaye Mungu akamtuma Sauli kwenda kuwahubiria wasio Wayahudi kuhusu Yesu na kuanzisha makanisa katika miji na vijiji mbalimbali. Wakati huu sasa akaanza kuitwa Paulo.
  • Paulo pia aliandika barua ili kuwatia moyo Wakristo katika makanisa kwenye miji hiyo. Barua hizi zipo katika agano jipya.