sw_tw/bible/names/paddanaram.md

13 lines
713 B
Markdown

# Padan-aramu
## Ufafanuzi
Padan-aramu lilikuwa jina la mji ambao familia ya Abrahamu waliishi kabla ya kuhamia kwenye nchi ya Kanaani. Inamaanisha "uwazi wa Aramu."
* Abrahamu alipoondoka Harani kule Padan-aramu akasafiri kwenda nchi ya Kanaani watu wengi wa familia yake walibaki Harani.
* Miaka mingi baadae mtumishi wa Abrahamu alikwenda Padan-aramu kutafuta mke kwa ajili ya Isaka miongoni mwa ndugu zake na akampata Rebeka, mjukuu wa Bethueli.
* Pia mtoto wa Isaka na Rebeka Yakobo alisafiri mpaka Padan-aramu na kuoa mabinti wawili wa kaka yake na Rebeka, Labani aliyekuwa akiishi Harani.
Aramu, Padan-aramu na Aramu-Nahariamu zilikuwa sehemu za mji mmoja ambao kwa sasa ni zipo katika nchi ya Syria.