sw_tw/bible/names/paddanaram.md

713 B

Padan-aramu

Ufafanuzi

Padan-aramu lilikuwa jina la mji ambao familia ya Abrahamu waliishi kabla ya kuhamia kwenye nchi ya Kanaani. Inamaanisha "uwazi wa Aramu."

  • Abrahamu alipoondoka Harani kule Padan-aramu akasafiri kwenda nchi ya Kanaani watu wengi wa familia yake walibaki Harani.
  • Miaka mingi baadae mtumishi wa Abrahamu alikwenda Padan-aramu kutafuta mke kwa ajili ya Isaka miongoni mwa ndugu zake na akampata Rebeka, mjukuu wa Bethueli.
  • Pia mtoto wa Isaka na Rebeka Yakobo alisafiri mpaka Padan-aramu na kuoa mabinti wawili wa kaka yake na Rebeka, Labani aliyekuwa akiishi Harani.

Aramu, Padan-aramu na Aramu-Nahariamu zilikuwa sehemu za mji mmoja ambao kwa sasa ni zipo katika nchi ya Syria.