13 lines
824 B
Markdown
13 lines
824 B
Markdown
# Ayubu
|
|
|
|
## Ufafanuzi
|
|
|
|
Ayubu alikuwa mtu anayeelezwa katika Biblia kama mtu asiye na hatia na mwenye haki mbele ya Mungu. Anajulikana zaidi kwa kutunza imani yake katika Mungu katika nyakati za mateso makali.
|
|
|
|
Ayubu aliishi katika nchi ya Usi iliyokuwa sehemu ndani ya nchi ya Kanaani, inawezekana katika maeneo ya Edomu.
|
|
Inafikiriwa kuwa aliishi wakati wa Esau na Yakobo kwa sababu mmoja wa marafiki wa Ayubu alikuwa "Mtemani," ambalo lilikuwa jina la kundi lililoitwa baada ya mjukuu wa Esau.
|
|
Kitabu cha Agano la Kale cha Ayubu kinaelezea jinsi Ayubu na wengine walivyoitikia mateso yake. Pia inatoa mtazamo wa Mungu kama muumbaji mwenye enzi na mtawala wa ulimwengu.
|
|
Baada ya maafa hayo yote, hatimaye Mungu alimponya Ayubu na kumpa watoto wengine na utajiri.
|
|
Kitabu cha Ayubu kinasema kuwa alikuwa mzee sana alipokufa.
|
|
|