sw_tw/bible/names/job.md

824 B

Ayubu

Ufafanuzi

Ayubu alikuwa mtu anayeelezwa katika Biblia kama mtu asiye na hatia na mwenye haki mbele ya Mungu. Anajulikana zaidi kwa kutunza imani yake katika Mungu katika nyakati za mateso makali.

Ayubu aliishi katika nchi ya Usi iliyokuwa sehemu ndani ya nchi ya Kanaani, inawezekana katika maeneo ya Edomu. Inafikiriwa kuwa aliishi wakati wa Esau na Yakobo kwa sababu mmoja wa marafiki wa Ayubu alikuwa "Mtemani," ambalo lilikuwa jina la kundi lililoitwa baada ya mjukuu wa Esau. Kitabu cha Agano la Kale cha Ayubu kinaelezea jinsi Ayubu na wengine walivyoitikia mateso yake. Pia inatoa mtazamo wa Mungu kama muumbaji mwenye enzi na mtawala wa ulimwengu. Baada ya maafa hayo yote, hatimaye Mungu alimponya Ayubu na kumpa watoto wengine na utajiri. Kitabu cha Ayubu kinasema kuwa alikuwa mzee sana alipokufa.