12 lines
744 B
Markdown
12 lines
744 B
Markdown
# Mhiti
|
|
|
|
## Ufafanuzi
|
|
|
|
Wahiti walikuwa ni uzao wa Hamu kupitia kwa mtoto wake Kanaani. Walifanyika kuwa dola kubwa katika eneo ambalo kwa sasa linaitwa Uturuki na Kaskazini mwa Palestina.
|
|
Ibrahimu alinunua sehemu ya ardhi kutoka kwa Efroni, Mhiti ili aweze kumzika Sara katika pango huko. Hatimaye, Ibrahimu na wazao wake kadhaa walizikwa katika pango hilo pia.
|
|
Wazazi wa Esau walihuzunika sana baada ya Esau kuoa wanawake Wahiti.
|
|
Mmoja kati ya watu wa Daudi aliyekuwa na nguvu aliitwa Uria Mhiti.
|
|
Miongoni mwa wanawake aliowaoa Sulemani walikuwa ni Wahiti. Wanawake hawa wa kigeni waliugeuza moyo wa Sulemani kutoka kwa Mungu kwasababu ya miungu waliyoiabudu.
|
|
Wahiti walikuwa mara zote ni hofu kwa waisraeli, kimwili na kiroho pia.
|
|
|