sw_tw/bible/names/cyprus.md

11 lines
524 B
Markdown

# Kipro
## Ufafanuzi
Kipro ni kisiwa katika bahari ya Mediteraniani karibu kilometa 64 kusini mwa nchi ya sasa ya Uturuki.
* Barnaba alikuwa anatokea Kipro hivyo inawezekana binamu yake Johana Marko alitokea huko pia.
* Paulo na Barnaba walihubiri kwa pamoja katika kisiwa cha Kipro katika mwanzo wa safari yao ya Kimisionari. Yohana Marko alikuja baadaye kuwasaidia katika safari zao.
* Baadae Barnaba na Marko walitembelea tena Kipro. Katika agano la kale Kipro imetajwa kama eneo lenye utajiri wa miti ya Miteashuri.