sw_tw/bible/names/cyprus.md

524 B

Kipro

Ufafanuzi

Kipro ni kisiwa katika bahari ya Mediteraniani karibu kilometa 64 kusini mwa nchi ya sasa ya Uturuki.

  • Barnaba alikuwa anatokea Kipro hivyo inawezekana binamu yake Johana Marko alitokea huko pia.
  • Paulo na Barnaba walihubiri kwa pamoja katika kisiwa cha Kipro katika mwanzo wa safari yao ya Kimisionari. Yohana Marko alikuja baadaye kuwasaidia katika safari zao.
  • Baadae Barnaba na Marko walitembelea tena Kipro. Katika agano la kale Kipro imetajwa kama eneo lenye utajiri wa miti ya Miteashuri.