sw_tw/bible/names/benaiah.md

456 B

Benaya

Ufafanuzi

Benaya lilikuwa jina la watu kadhaa katika Agano la Kale.

  • Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa miongoni mwa mashujaa wa Daudi. Alikuwa shujaa mwenye ujuzi na aliwekwa kuwa mlinzi wa Daudi.
  • Sulemani alipotawazwa kuwa mfalme, Benaya alimsaidia kuwaaribu adui zake, hatimaye akawa jemedari wa jeshi la Israeli.
  • Watu wengine wenye jina Benaya katika Agano la Kale ni pamoja na Walawi watatu: kuhani, mwimbaji, na mwana wa Asafu.