sw_tw/bible/names/baasha.md

12 lines
557 B
Markdown

# Baasha
## Ufafanuzi
Baasha alikuwa miongoni mwa wafalme waovu wa Israeli,waliowashawishi Waisraeli kuabudu vinyago.
* Baasha alikuwa mfalme wa tatu wa Israeli na alimiliki kwa miaka ishirini na minne, wakati Asa akiwa mfalme wa Yuda.
* Alikuwa jemedari wa jeshi aliyejifanya mfalme baada ya kumwua mfalme Nadabu, mtangulizi wake.
* Kulikuwa na mapigano mengi wakati wa utawala wa Baasha kati ya ufalme wa Israeli na Yuda, hasa na Asa mfalme wa Yuda.
* Dhambi nyingi alizozitenda Baasha hatimaye zilimfanya Mungu kumwondoa katika nafasi yake kwa kifo.