557 B
557 B
Baasha
Ufafanuzi
Baasha alikuwa miongoni mwa wafalme waovu wa Israeli,waliowashawishi Waisraeli kuabudu vinyago.
- Baasha alikuwa mfalme wa tatu wa Israeli na alimiliki kwa miaka ishirini na minne, wakati Asa akiwa mfalme wa Yuda.
- Alikuwa jemedari wa jeshi aliyejifanya mfalme baada ya kumwua mfalme Nadabu, mtangulizi wake.
- Kulikuwa na mapigano mengi wakati wa utawala wa Baasha kati ya ufalme wa Israeli na Yuda, hasa na Asa mfalme wa Yuda.
- Dhambi nyingi alizozitenda Baasha hatimaye zilimfanya Mungu kumwondoa katika nafasi yake kwa kifo.