sw_tw/bible/names/aram.md

15 lines
842 B
Markdown

# Arami, Waarami
## Ufafanuzi
"Arami" ni jina la watu wawili katika agano la kale. Pia lilikuwa jina la mji uliopo kaskazini mashariki mwa Kaanani, ambayo kwa sasa ni Siria.
* Watu wanaoishi Arami wanajulikana kama Waarami wanaozungumza Kiarami. Yesu na Wayahudi wengine pia walizungumza Kiarami.
* Moja ya watoto wa Shemu aliitwa Arami. Mtu mwingine aliyeitwa Arami alikuwa binamu yake na Rebeka.
* Arami baadaye ikaja kujulikana kwa jina la Kigiriki kama Siria.
* "Padani Arami" ina maanisha "Tambarare ya Arami" na ilikuwa kaskazini mwa Arami.
* Baadhi ya ndugu wa Abrahamu walioishi Harani ambayo ilikuwepo Padani Arami.
* Katika agano la kale neno Arami na Padani Arami linamaanisha sehemu moja.
* Neno "Arami Naharaimu" ina maana ya "Arami ya mito miwili" Mji huu ulikuwepo Kaskazini mwa Mesopitamia na mashariki mwa Padani Arami.