sw_tw/bible/names/aram.md

842 B

Arami, Waarami

Ufafanuzi

"Arami" ni jina la watu wawili katika agano la kale. Pia lilikuwa jina la mji uliopo kaskazini mashariki mwa Kaanani, ambayo kwa sasa ni Siria.

  • Watu wanaoishi Arami wanajulikana kama Waarami wanaozungumza Kiarami. Yesu na Wayahudi wengine pia walizungumza Kiarami.
  • Moja ya watoto wa Shemu aliitwa Arami. Mtu mwingine aliyeitwa Arami alikuwa binamu yake na Rebeka.
  • Arami baadaye ikaja kujulikana kwa jina la Kigiriki kama Siria.
  • "Padani Arami" ina maanisha "Tambarare ya Arami" na ilikuwa kaskazini mwa Arami.
  • Baadhi ya ndugu wa Abrahamu walioishi Harani ambayo ilikuwepo Padani Arami.
  • Katika agano la kale neno Arami na Padani Arami linamaanisha sehemu moja.
  • Neno "Arami Naharaimu" ina maana ya "Arami ya mito miwili" Mji huu ulikuwepo Kaskazini mwa Mesopitamia na mashariki mwa Padani Arami.