sw_tw/bible/kt/sanctify.md

11 lines
461 B
Markdown

# takasa, utakaso
## Ufafanuzi
Kutakasa ni kutenga kando au kufanya takatifu. Utakaso ni hatua ya kufanya takatifu.
* Katika Agano la Kale, baadhi ya watu na vitu vilitakaswa, au kutengwa kando, kwa hudumu ya Mungu.
* Agano Jipya lina fundisha kuwa Mungu anatakasa watu wanao mwamini Yesu. Hiyo ni kwamba, anawafanya watakatifu na kuwatenga kumtumikia.
* Waamini katika Yesu wanaamriwa kujitakasa kwa Mungu, kuwa watakatifu katika kila kitu wanacho fanya.