sw_tw/bible/kt/reconcile.md

11 lines
489 B
Markdown

# Kupatanisha, maridhiano
## Ufafanuzi
Kupatanisha na maridhiano ni kutengeneza amani kati ya watu waliokuwa maadui.
* Katika Biblia neno hili linamuelezea Mungu kuwapatanisha watu na yeye mwenyewe kwa kumtoa mwana wake Yesu Kristo.
* Kwa sababu ya dhambi watu wote ni adui wa Mungu. Lakini kwa sababu ya upendo wake Mungu anatoa njia ya watu kupatanishwa naye kupitia Yesu.
* Kwa kuamini kujitoa kwa Yesu kama malipo ya dhambi zao watu wanaweza kusamehewa na kuwa na amani na Mungu.