sw_tw/bible/kt/prophet.md

16 lines
773 B
Markdown

# Nabii, unabii, mwonaji, nabii mwanamke.
## Ufafanuzi
"Nabii ni mtu anayesema ujumbe wa Mungu kwa watu. Mwanamke anayefanya hivi anaitwa "nabii mwanamke."
* Mara nyingi manabii waliwaonya watu kuacha dhambi zao na kumtii Mungu.
* Unabii ni ujumbe unaozungumzwa na nabii.
* Ujumbe wa unabii mara nyingi ulikuwa unahusu mambo yatakayotokea hapo baadae.
* Unabii mwingi wa agano la kale umeshatimia.
* Katika Biblia mkusanyiko wa vitabu vilivyoandikwa na manabii mara nyingine vinajulikana kama "manabii."
* Kwa mfano maneno "sheria na manabii" ni namna ya kuelezea maandiko ya kiebrania ambayo yanajulikana kama "agano la kale"
* Jina la zamani la nabii lilikuwa "mwonaji" au "mtu anayeona."
* Mara nyingine "mwonaji" inamana ya nabii wa uongo au mtu anayefanya uganga.