sw_tw/bible/kt/prophet.md

773 B

Nabii, unabii, mwonaji, nabii mwanamke.

Ufafanuzi

"Nabii ni mtu anayesema ujumbe wa Mungu kwa watu. Mwanamke anayefanya hivi anaitwa "nabii mwanamke."

  • Mara nyingi manabii waliwaonya watu kuacha dhambi zao na kumtii Mungu.
  • Unabii ni ujumbe unaozungumzwa na nabii.
  • Ujumbe wa unabii mara nyingi ulikuwa unahusu mambo yatakayotokea hapo baadae.
  • Unabii mwingi wa agano la kale umeshatimia.
  • Katika Biblia mkusanyiko wa vitabu vilivyoandikwa na manabii mara nyingine vinajulikana kama "manabii."
  • Kwa mfano maneno "sheria na manabii" ni namna ya kuelezea maandiko ya kiebrania ambayo yanajulikana kama "agano la kale"
  • Jina la zamani la nabii lilikuwa "mwonaji" au "mtu anayeona."
  • Mara nyingine "mwonaji" inamana ya nabii wa uongo au mtu anayefanya uganga.