19 lines
1.2 KiB
Markdown
19 lines
1.2 KiB
Markdown
# Moyo
|
|
|
|
## Ufafanuzi
|
|
|
|
Katika Biblia, neno 'moyo' limetumika mara nyingi kimfano kurejelea mawazo ya mtu, hisia, tamaa au utashi.
|
|
Kuwa na 'moyo mgumu' ni msemo wa kawaida wenye maana ya mtu anayemwasi Mungu kwa ukaidi.
|
|
Msemo "kwa moyo wote'' au '' kwa moyo wangu wote'' una maana ya kufanya kitu kwa kujitoa kikamilifu na kwa uhiari.
|
|
Msemo mwingine '' weka moyoni" una maana kuchukulia kitu kwa umakini na kukitumia katika maisha.
|
|
Maneno " kuvunjika moyo'' humwelezea mtu ambaye ana huzuni. Wamekuwa wameumizwa kihisia za ndani
|
|
|
|
Mapendekezo ya tafsiri
|
|
Baadhi ya lugha hutumia sehemu tofauti za mwili kama vile 'tumbo' au 'ini' kurejelea mawazo haya.
|
|
Lugha zingine zaweza kutumia neno moja kuelezea dhana hizi na neno jingine kueleza dhana zingine.
|
|
kama 'moyo' au sehemu nyingine ya mwili haina maana hii, lugha zingine zaweza kuhitaji kutumia maneno ya moja kwa moja kama vile 'fikra' au 'hisia' au 'tamaa.'
|
|
Kwa kutegemeana na muktadha, maneno "kwa moyo wangu wote" yaweza kutafsiriwa kama "kwa nguvu zangu zote" au "kwa kujitoa kimamilfu"
|
|
Maneno kama "weka moyoni" yaweza kutafsiriwa kama 'shughulikia kwa umakini' au fikiria kwa uangalifu"
|
|
"kuvunjika moyo" ina maana ya kuwa 'mwenye huzuni' au 'kujisikia kuumizwa kwa ndani"
|
|
|