sw_tw/bible/kt/covenant.md

14 lines
703 B
Markdown

# Agano
## Ufafanuzi
Agano ni makubaliano kati ya pande mbili kuwa upande mmoja au zote unapaswa kutekeleza.
* Makubaliano haya yanaweza kuwa ya mmoja mmoja, kati ya makundi ya watu au kati ya Mungu na watu.
* Watu wanapoweka agano kati yao wanaahidi kufanya jambpo fulani ambalo wanapaswa wafanye.
* Mfano wa maagano ya wanadamu ni maagano ya ndoa, makubaliano ya biashara na mikataba kati ya nchi.
* Katika Biblia Mungu ameweka maagano mbalimbali na watu wake.
* Katika baadhi ya maagano Mungu aliahidi kutekeleza bila masharti yoyote. Kwa mfano Mungu alipoweka agano na mwanadamu kuwa hataiangamiza duinia kwa mafuriko.
* Katika maagano mengine Mungu ameahidi kutekeleza kama watu watamtii yeye.