703 B
703 B
Agano
Ufafanuzi
Agano ni makubaliano kati ya pande mbili kuwa upande mmoja au zote unapaswa kutekeleza.
- Makubaliano haya yanaweza kuwa ya mmoja mmoja, kati ya makundi ya watu au kati ya Mungu na watu.
- Watu wanapoweka agano kati yao wanaahidi kufanya jambpo fulani ambalo wanapaswa wafanye.
- Mfano wa maagano ya wanadamu ni maagano ya ndoa, makubaliano ya biashara na mikataba kati ya nchi.
- Katika Biblia Mungu ameweka maagano mbalimbali na watu wake.
- Katika baadhi ya maagano Mungu aliahidi kutekeleza bila masharti yoyote. Kwa mfano Mungu alipoweka agano na mwanadamu kuwa hataiangamiza duinia kwa mafuriko.
- Katika maagano mengine Mungu ameahidi kutekeleza kama watu watamtii yeye.