sw_tw/bible/kt/confess.md

13 lines
636 B
Markdown

# Kukiri
## Ufafanuzi
Kukiri inamaana ya kukubali kuwa jambo fulani ni la kweli. Kukiri ni kauli ya kuwa kitu fulani ni kweli.
* Kukiri pia yaweza kuwa na maana ya kusema ukweli kuhusu Mungu. Pia yaweza kuonesha kukubali kuwa sisi ni wenye dhambi.
* Biblia inasema watu wakikiri dhambi zao kwa Mungu atawasamehe.
* Mtume Yakobo aliandika kwenye barua yake kuwa waamini wakikiri dhambi zao wao wenyewe inawaletea uponyaji wa kiroho.
* Mtume Paulo aliwaandikia Wafilipi kuwa siku moja kila mtu atakiri kuwa Yesu ni Bwana.
* Paulo pia anasema watu wakikiri kuwa Yesu ni Bwana na kuamini kuwa Mungu alimfufua toka kwa wafu wataokolewa.