sw_tw/bible/kt/confess.md

636 B

Kukiri

Ufafanuzi

Kukiri inamaana ya kukubali kuwa jambo fulani ni la kweli. Kukiri ni kauli ya kuwa kitu fulani ni kweli.

  • Kukiri pia yaweza kuwa na maana ya kusema ukweli kuhusu Mungu. Pia yaweza kuonesha kukubali kuwa sisi ni wenye dhambi.
  • Biblia inasema watu wakikiri dhambi zao kwa Mungu atawasamehe.
  • Mtume Yakobo aliandika kwenye barua yake kuwa waamini wakikiri dhambi zao wao wenyewe inawaletea uponyaji wa kiroho.
  • Mtume Paulo aliwaandikia Wafilipi kuwa siku moja kila mtu atakiri kuwa Yesu ni Bwana.
  • Paulo pia anasema watu wakikiri kuwa Yesu ni Bwana na kuamini kuwa Mungu alimfufua toka kwa wafu wataokolewa.