sw_tw/bible/kt/christian.md

12 lines
586 B
Markdown

# Mkristo
## Ufafanuzi
Baada ya Yesu kurudi mbinguni watu wakaanza kuitwa Wakristo ikiwa na maana ya wafuasi wa Kristo.
* Ilikuwa katika mji wa Antiokia ambapo wafuasi wa Yesu waliitwa Wakristo kwa mara ya kwanza.
* Mkristo ni mtu anayeamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu na anayeamini kuwa Yesu anaweza kumuokoa toka kwenye dhambi.
* Katika wakati wa sasa Mkristo ni mtu anayetambulishwa na dini ya Kikristo lakini sio mfuasi wa Yesu kabisa. Hii sio maana ya Mkristo ki Biblia.
* Kwa sabau Mkristo kwenye Biblia inamaanisha mtu anayemwamini Yesu kabisa Mkristo pia anaitwa mwamini.