sw_tw/bible/kt/blood.md

20 lines
1.1 KiB
Markdown

# damu
## Ufafanuzi
Neno "damu" linamaanisha kimiminika chekundu kinachotoka katika ngozi ya mtu panapokuwa na jeraha au kidonda. Damu inaleta viini lishe vya uhai katika mwili wote wa mtu.
* Damu inaashiria uhai na inapomwagwa, inaashiria kifo.
* Watu walipotoa sadaka kwa Mungu, walimwua mnyama na kumimina damu yake juu ya madhabahu. Hii inaashiria kutolewa kwa uhai wa mnyama kulipa dhambi za watu.
* Kupitia kifo chake msalabani, Damu ya Yesu hutakasa watu kutokana na dhambi zao na kulipa kwa ajili ya adhabu wanayostahili kwa ajili ya dhambi zao.
* Kifungu "mwili na damu" kinarejerea wanadamu.
* Kifungu "mwili wake na damu yake" inarejerea kwa watu wanaohusiana kibaolojia.
## Maoni ya Kutafasiri
* Neno hili litumika kwa kulingana na neno lifaalo katika lugha lengwa.
* Kielezi "mwili na damu" chaweza kutafasiriwa kama "watu" au "wanadamu".
* Kwa kutegemea mazingira, kifungu "mwili wangu na damu yangu mwenyewe" yaweza kutafasiriwa kama "familia yangu" au "ndugu zangu" au "watu wangu."
* Ikiwa kuna kionyeshi katika lugha lengwa kinachotumika kwa maana hii, kifungu hicho kitumike kutafasiri "mwili na damu"