sw_tw/bible/kt/atonement.md

11 lines
514 B
Markdown

# Upatanisho, kulipia
## Ufafanuzi
"Upatanisho au kulipia" inaonesha ni jinsi gani Mungu alitoa sadaka ili kulipia dhambi za watu.
* Katika agano la kale Mungu aliruhusu upatanisho wa muda ufanyike kwa ajili ya utakaso wa dhambi za wana wa Israeli, ambapo ilitolewa sadaka ya damu iliyohusisha kuchinjwa kwa mnyama.
* Katika agano jipya kifo cha Kristo msalabani ni upatanisho wa pekee na wa kudumu kwa ondoleo la dhambi.
* Yesu alipokufa alichukua adhabu ya watu waliostahili adhabu ile kwa sababu ya dhambi.