sw_tw/bible/kt/adultery.md

13 lines
576 B
Markdown

# Uzinzi, zinaa, mzinifu, mzinzi
## Ufafanuzi
Neno "uzinzi" hii ni dhambi ambayo inahusisha mwanandoa ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye sio mwenza wake.
* "Mzinifu" ni mtu yeyote anayefanya uzinzi.
* Mara nyingine mzinzi hutumika kuonesha kuwa ni mwanamke ndiye anayefanya uzinzi.
* Uzinzi huvunja ahadi ambayo mke na mume wamewekeana katika agano la ndoa.
* Mungu aliwaamuru Wana wa Israeli wasizini.
* Pia "zinaa" hutumika kama lugha ya picha kuwaelezea wana wa Israeli namna ambavyo hawakuwa waaminifu kwa Mungu, hasa walipokuwa wakiabudu miungu mingine.