sw_tw/bible/kt/adultery.md

576 B

Uzinzi, zinaa, mzinifu, mzinzi

Ufafanuzi

Neno "uzinzi" hii ni dhambi ambayo inahusisha mwanandoa ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye sio mwenza wake.

  • "Mzinifu" ni mtu yeyote anayefanya uzinzi.
  • Mara nyingine mzinzi hutumika kuonesha kuwa ni mwanamke ndiye anayefanya uzinzi.
  • Uzinzi huvunja ahadi ambayo mke na mume wamewekeana katika agano la ndoa.
  • Mungu aliwaamuru Wana wa Israeli wasizini.
  • Pia "zinaa" hutumika kama lugha ya picha kuwaelezea wana wa Israeli namna ambavyo hawakuwa waaminifu kwa Mungu, hasa walipokuwa wakiabudu miungu mingine.