sw_tw/bible/other/winepress.md

603 B

Shinikizo la divai

Ufafanuzi

Katika nyakati za Biblia shinikizo la divai ni vyombo vikubwa au sehemu ya wazi ambapo maji ya zabibu yalitengenezwa na kufanywa kuwa divai.

  • Katika Israeli shinikizo la divai lilikuwa beseni kubwa lililochimbwa kwenye mwamba. Na watu walikanyaga zabibu kwa miguu yao ili wapate maji ya zabibu.
  • Shinikizo la divai lilikuwa na hatua mbili, zabizu zilizokanyagwa kwenye hatua ya juu ili maji ya zabibu yatiririke chini kwenye hatua ya chini ambapo hukusanywa.
  • Pia shinikizo la divai limetumika kuonesha picha ya hasira ya Mungu atakayoimimina juu ya watu waovu.