sw_tw/bible/other/walk.md

509 B

Tembea

Ufafanuzi

Neno "tembea" mara nyingi hutumika ikiwa na maana ya "ishi."

  • "Enoko alitembea na Mungu" inamaanisha kuwa "Enoko aliishi kwa kuwa na mahusiano ya ukaribu sana na Mungu."
  • "Kutembea kwa roho" inamaanisha kuongozwa na Roho Mtakatifu ili kufanya mambo yanayomtukuza na kumpa heshima Mungu.
  • Mungu anaposema atatembea kati ya watu wake inamaana kuwa anaishi kati yao au anahusiana nao kwa karibu.
  • "Kutembea kinyume" inamaanisha kuwa kuishi au kufanya kinyume na mtu au kitu fulani.