sw_tw/bible/other/tent.md

873 B

hema

Ufafanuzi

Hema ni hifadhi linalo hama lililo tengenezwa na uzi uliyo zungushiwa kwenye nguzo pamoja.

  • Mahema yanaweza kuwa madogo, yenye kiasi cha nafasi cha watu kulala humo, au yanaweza kuwa makubwa, yenye nafasi ya familia nzima kulala, kupika, na kuishi.
  • Kwa watu wengi, mahema yanatumika kama sehemu ya kudumu ya kuishi. Kwa mfano, wakati wa muda mwingi familia ya Ibrahimu iliishi katika nchi ya Kanani, waliishi katika mahema makubwa yaliyo tengenezwa na nywele za mbuzi.
  • Waisraeli pia waliishi katika mahema kipindi cha miaka yao arobaini wakizunguka jangwa la Sinai.
  • Jengo la maskani lilikuwa aina ya hema kubwa, yenye kuta nene zilizo tengenezwa na vitambaa.
  • Wakati mtume Paulo alipo safiri miji tofauti kueneza injili, alifanya mahema kupata pesa kujikimu.
  • Wakati mwingine neno "hema" linaweza tumika kifumbo kueleza wapi watu wanaishi.