sw_tw/bible/other/servant.md

1.2 KiB

mtumishi, mtumwa, utumwa

Ufafanuzi

Neno "mtumishi" la weza pia maanisha "mtumwa" na kumueleza mtu anaye mfanyia mtu mwingine kazi, iwe kwa uwamuzi au kwa lazima. Muktadha wa maneno yaliyo zunguka yanaweka dhahiri kuwa kama mtumishi au mtumwa ndiye anaye tajwa.

  • Katika nyakati za Biblia, kulikuwa na tofauti ndogo katika ya mtumishi na mtumwa kuliko ilivyo leo. Wote watumishi na watumwa walikuwa sehemu muhimu ya nyumba ya bwana wao na wengi walichukuliwa kama ndugu wa familia.
  • Mtumwa ni aina ya mtumishi ambaye ni mali ya mtu anaye mfanyia kazi. Mtu anaye nunua mtumwa anaitwa "mmiliki" au "bwana." Mabwana wengine wanawatendea watumwa wao kwa ukatili sana, wakati wengine wana watendea vizuri.
  • Zamani za kale, watu wengine kwa hiari walikuwa watumwa kwa mtu aliye wadai ilikulipa deni lao.
  • Katika Biblia, maneno "mimi ni mtumishi wako" yalitumika kama alama ya heshima na huduma kwa mtu wa ngazi ya juu, kama mfalme. Haimanishi kwamba mtu anaye zungumza alikuwa mtumishi halisi.
  • Katika Agano la Kale, manabii wa Mungu na watu wengine waliyo muabudu Mungu mara nyingi waliitwa "watumishi."
  • Wakristo pia wanaitwa "watumwa wa haki," ambayo ni mfano unao linganisha uwaminifu wa kumtii Mungu kama mtu anavyo mtii bwana wake.