sw_tw/bible/other/seed.md

702 B

mbegu, manii

Ufafanuzi

Mbegu ni sehemu ya mmea unao oteshwa kwenye ardhi kuzalisha aina moja zaidi ya mmea huo. Pia ina maana kadha ya mafumbo.

  • Neno "mbegu" linatumika kwa fumbo na tafsida kuelezea seli ndogo ndani ya mwanaume au mwanamke zinazo jumuika kusababisha mtoto kukua ndani ya mwanamke, hii ina itwa manii.
  • Pamoja na hii, "mbegu" inatumika kueleza uzao wa mtu.
  • Neno hili lina maana ya wingi, likieleza zaidi ya mbegu moja au zaidi ya mzao mmoja.
  • Katika mfano wa mkulima akipanda mbegu, Yesu alifananisha mbegu na Neno la Mungu lililo pandwa katika mioyo ya watu ilikuweza kuzalisha matunda mazuri ya kiroho.
  • Mtume Paulo pia anatumia neno "mbegu" kumaanisha Neno la Mungu.