657 B
657 B
fimbo ya kifalme
Ufafanuzi
Neno "fimbo ya kifalme" ina husu gongo zuri linalo shikiliwa na mtawala, kama mfalme.
- Fimbo hizi zilikuwa tawi la mbao lenye mapindo ya mapambo. Baadae fimbo za kifalme zilitengenezwa kwa vyuma vya dhahabu.
- Fimbo ya kifalme ilikuwa alama ya ufalme na mamlaka iliyo hashiria heshima na ukuu wa mfalme.
- Katika Agano la Kale, Mungu anaelezwa kuwa na fimbo ya haki. Hii ina husu Mungu kutawala kama mfalme wa watu wake.
- Unabii wa Agano la Kale kuhusu Mesiya unamueleza kuwa kama mfano wa fimbo ambayo itakuja kutoka Israeli kutawala mataifa yote.
- Hii yaweza tafsiriwa kama, "gongo la utawala" au "gongo la mfalme."